GSK yatuhumiwa kuwahonga madaktari

Haki miliki ya picha Getty
Image caption GSK inatoa ushirikiano katika uchunguzi unaoendelea

Uchunguzi wa kipindi cha BBC Panorama unafichua kuwa kampuni ya madawa Uingereza GlaxoSmithKline inakabiliwa na uchunguzi wa kihalifu nchini Poland kwa kutuhumiwa kuwahonga madaktari.

Madaktari kumi na moja na mkurugenzi wa tawi la kampuni hiyo wameshtakiwa kwa rushwa kati ya mwaka 2010 na 2012.

Afisa mmoja anayehusika na uuzaji wa dawa za kampuni hiyo amesema madaktari walilipwa kushinikiza mauzo ya dawa ya pumu Seretide ya kampuni hiyo ya GSK.

Kwa upande wake GSK inasema imemuadhibu mfanyakazi mmoja na inatoa ushirikiano katika uchunguzi unaoendelea.

Iwapo tuhuma hizo zitathibitishwa, huenda GSK imekiuka sheria inayopinga rushwa Uingereza na sheria ya Marekani inayoharamisha rushwa katika nchi za nje. Ni haramu kwa kampuni zilizopo nchini kuwahonga wafanyakazi wa serikali katika nchi za nje.

Image caption Dawa ya pumu Seretide ya kampuni ya GSK.

Daktari mmoja amekiri kufanya makosa, na ametozwa faini na amecheleweshwa kifungo. Alikiri kupokea pauni 100 kutokana na shinikizo la mwakilishi wa GSK, kwa malipo ya uhamasisho kuhusu dawa hizo ambao hakuutoa.

Akosolewa na Kuadhibiwa

GSK imegundua utovu wa mawasiliano uliotekelezwa na mfanyakazi mmoja ambao ni kinyume na sera za kampuni hiyo katika mafunzo ya kuimarisha viwango vya utafiti na mafunzo ya kiafya kuhusu magonjwa ya kupumua yaliotoloewa na madaktari kati ya mwaka 2010 hadi 2012.

GSK ilifanya uchunguzi wa ndani na nje ya kampuni hiyo baada ya kupokea tuhuma kadhaa kuhusu jinsi mafunzo hayo yanavyotolewa katika eneo la Lodz.

GSK inasema: "Tunaendelea kuchunguza haya mambo na tunashirikiana kikamilifu na CBA". Ofisi kuu nchini Poland inayokabiliana na rushwa.

Mnamo 2012, GSK ililipa $ bilioni 3bn (£ bilioni 1.9) I katika kesi kbwa ya udanganyifu katika sekta ya afya katika historia ya Marekani, baada ya kukiri makosa ya kuuza dawa mbili kwa matumizi ambayo hayajaidhinishwa na kutoripoti kuhusu usalama wa kutumia dawa ya kisukari kwa taasisi ya vyakula na madawa nchini.