Arsenal yailaza West Ham

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsenal 3-1 West ham

Lukas Podolski alifunga mabao mawili na kuisaidia Arsenal kutoka nyuma na kuilaza West Ham,3-1.

West Ham ndio walioanza kufunga bao la kwanza, kupitia kwa Matt Jarvis kunako dakika ya 40 ya kipindi cha kwanza .

hata hivyo furaha ya West ham ilidumu kwa dakika nne tu kwani hata kabla kivumbi hakijatua Lukas Podolski aliisawazishia Arsenal na kuwapa the gunners fursa ya kusitisha msururu wa matokeo duni .

Ganga ganga ya mapumzikoni ilipelekea vijana wa Arsene Wenger kufunga bao la pili na kuongoza kwa mara ya kwanza katika mechi hiyo kupitia kwa Olivier Giroud.

Masaibu ya West ham yalizidi Podolski alipofunga bao la tatu na ushindi na kuisaidia Arsenal kuipiku Everton katika nafasi ya nne katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza..

Hata hivyo Wenger atasubiri na kuomba Everton ikunguwae dhidi ya Crystal palace katika mechi yao itakayochezwa baadaye leo jioni.

Man City Inakungutana na Sunderland katika mechi nyengine ya katikati ya wiki..