Rais Bouteflika kugombea Urais Algeria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Bouteflika anaugua kiharusi

Wananchi wa Algeria leo wanapiga kura kumchagua Rais mpya. Rais wa sasa Abdelaziz Bouteflika anawania kwa muhula wa nne.

Bwana Bouteflika, mwenye umri wa miaka 77, hajaonekana sana hadharani tangu kupatwa na kiharusi mwaka jana.

Pia hajaonekana akifanya kampeini zake hadharani.

Uchaguzi huo unashirkisha wagombea sita.

Upinzani umefanya maandamano ya kuupinga uchaguzi huo na kuwataka watu kuasusia wakiutaja kama kiini macho.

Wanasema kuwa Bouteflika hana uwezo wa kugombea kwa sababu ya afya yake mbaya.