Bouteflika ashinda uchaguzi Algeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bouteflika amekuwa akiugua Kiharusi kwa miaka mingi

Taarifa kutoka nchini Algeria zinasema kuwa Rais Abdelaziz Bouteflika ameshinda uchaguzi mkuu uliofanyika mnamo siku ya Alhamisi.

Bouteflika alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 80 ya kura na kupata nafasi ya kuongoza kwa muhula wa nne.

Hata kabla ya matokeo kutangazwa, kiongozi wa chama rasmi cha upinzani Ali Benflis, alisema kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na wizi.

Bouteflika, ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka 15, anakumbwa na hali mbaya ya kiafya kwani anaugua kiharusi na alipiga kura akiwa katika kiti cha magurudumu.