Maafikiano kukomesha uhasama Ukraine

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Maafikiano kukomesha uhasama Ukraine

Baada ya vuta ni kuvute sasa Wawakilishi wa Marekani, Muungano wa Ulaya,pamoja na mawaziri wa kigeni wa Ukraine na Urusi wameafikiana kuwa makundi yote ya kijeshi yaliyoko Ukraine bila idhini, yanafaa

kunyang'anywa silaha na kuondoka mara moja kwenye majengo ya serikali wanayoyadhibiti mashariki mwa Ukraine.

Waziri wa maswala ya kigeni wa Urusi Sergey Lavrov aliwataka waasi waondoke kutoka kwenye majengo ya serikali ya Ukraine katika miji iliyoko mashariki mwa Ukraine

Lavrov aliwaambia waandishi wa habari baada ya mazungumzo ''Baada ya Mazungumzo kati yetu tumekubaliana kuwa wapiganaji ambao si wakijeshi waondoke katika majengo yote ya serikali .

Ningependa kila mtu anayemiliki silaha aisalimishe kwa serikali yana atapewa msamaha'' .

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry ametaja mkutano huo kama "siku njema na yenye ufanisi mkubwa ''.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maafikiano kukomesha uhasama Ukraine

Hata hivyo Rais wa Marekani Barrack Obama amesema kuwa hana jingine ila kuzidisha vikwazo dhidi ya Urusi iwapo Moscow itaendelea kukiuka makubaliano.

''hadi kufikia sasa Tutayafuatilia walichokubaliana kwa siku chache zijazo hata hivyo nimezungumza na Chansela Angela Merkel na pia waziri mkuu wa Uingereza David Cameron na viongozi wengine wa bara Ulaya ilikuhakiki

vikwazo zaidi iwapo urusi itakiuka walichoafikiana

Naye Waziri wa Nchi za kigeni wa Ukraine', Andriy Deshchytsia, amesema kuwa anapingana na Urusi katika misingi kadhaa ikiwemo chanzo za mzozo huo, lakini taifa lake litatekeleza yote yaliyoafikiwa.

''Tunatoofautiana pakubwa na Urusi katika maswala mengi tu lakini ningependa kukubaliana na urusi katika makubaliano ya leo ningependa kuipa fursa Urusi ya kusitisha juhudi za kuigawanya Ukraine''.