Mjumbe wa Iran azuiwa kungia Marekani

Haki miliki ya picha Getty

Rais Obama ametia sahihi mswada unaomzuia balozi mteule wa Iran katika umoja wa mataifa kuchukua wadhfa wake mjini New York.

Ikulu ya whiteshouse tayari ilikuwa imetangaza kuwa mwanadiplomasia huyo mwenye uzoefu mkubwa Hamid Abutalebi,hatapewa Viza.

Bwana Abutalebi anashirikishwa na utekaji wa ubalozi wa Marekani nchini Iran mnamo mwaka 1979,ijapokuwa amesisitiza kuwa alikuwa mkalimani wa watekaji hao.

Iran imesema kuwa Marekani haiwezi kumzuia mjumbe wa umoja wa mataifa kutekeleza wajibu wake.

Bunge la Congress lilipitisha mswada huo ili kumzuia mtu yeyote anayashukiwa kujihusisha na upelelezi ama ugaidi dhidi ya Marekani ama mtu ambaye ni tishio kwa usalama wa taifa hilo.