'Heartbleed' hatari kwa mtandao

Ladar Levison amepoteza vita vyake vya hivi punde dhidi ya FBI.

Mwanzilishi wa mfumo wa huduma za baruapepe wa, Lavabit, ambao ulitumiwa na Edward Snowden, alikuwa akipinga uamuzi uliosema kuwa alikataa kutoa funguo za mfumo huo katika ukurasa wake.

Levison aliiambia makala ya bbc ya teknolojia 'Click' mapema mwaka huu kuwa kutoa funguo hizo ni sawa na kuruhusu serikali ya Marekani kuingia katika mtandao wa Lavabits unaohifadhi data za watumizi laki nne.

Haki miliki ya picha other
Image caption MtGox

MtGox (PRON Mount Gox), Iliyokuwa kwa wakati mmoja kampuni kubwa ya ubadilishanaji ulimwenguni ya Bitcoin imewekwa chini ya usimamizi na mahakama ya Japan.

Kubadilishana huko kulikotangazwa Februari kulionesha kuwa wadukuzi walikuwa wameiba maelfu ya chembechembe za bitcoins zinazogharimu takriban dola milioni 500.

Wanaotarajia kurejeshewa hela zao wameombwa kuuliza malipo yao kupitia kwa mahakama japokuwa kufikia sasa hakuna muda maalum uliotengwa kwa utaratibu huo.

Image caption Chrome

Jitayarishe kuharibu vipindi vya televisheni vinavyoudhi ikiwa unatumia mtandao wa Chrome.

Upo mfumo mpya ungamanishi unaoitwa Silencer ambao unaruhusu watumizi kutumia vidude maalum vya hash, maneno na vifungu ambavyo vitafutwa katika taarifa zinazowekwa kwa Twitter na Facebook.

Kwa hivyo wakati mwingine kukiwa na ndoa Westeros (PRON Wester-Ross), watumiza watahakikishiwa usumbufu wanaposakura mtandao hadi watakapoelewa mambo.

Haki miliki ya picha Heartbleed.com
Image caption Heartbleed

Tovuti ya Heartbleed inaendelea kuleta matatizo katika mfumo mzima wa tovuti.

Halmashauri ya ukusanyaji ushuru ya Canada na na mtandao wa Mumsnet, unatumiwa na wazazi Uingereza, zote zilitangaza wiki hii kuwa data zao zilikuwa zimeibwa na wadukuzi waliokuwa wakitalii tovuti ya Heartbleed .

Wezi wa mitandao walipata nambari za siri na jumbe kutoka katika mtandao Mumsnet ulipokuwa ukitengenezwa wakati halmashauri ya ushuru ya Canada ikisema kuwa zaidi ya nambari 900 za bima za kijamii za watu zilikuwa zimeibwa.