Aponea kifo kwenye gurudumu la ndege

Image caption Karibu robo ya watu wote wanaosafiri wakiwa wamejificha katika gurudumu la ndege hufariki

Mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 16 amenusurika kifo kwa maajabu baada ya kujificha na kusafiri katika gurudumu la ndege iliyokuwa ikielekea mjini Carlifornia kutoka Hawaii nchini Marekani.

Safari hiyo ilidumu kwa saa 5.

Hali yake inadaiwa kuwa shwari licha ya vipimo vya juu vya baridi baada ya ndege hiyo kusafiri juu ya bahari ya Pacifiki kwa saa tano.

Msemaji wa shirika la ndege la Hawaii, alisema kuwa wafanyakazi wa shirika hilo walimuona kijana huyo baada ya ndege kutua Jumapili asubuhi.

Alihojiwa na FBI na kupewa huduma ya dharura huku wauguzi wakisema afya yake iko shwari.

Mvulana huyo anasemekana kutoroka nyumbani na kuruka ukuta katika uwanja wa San Jose ili kuweza kusafiri kwa ndege hiyo.

''Wasiwasi wetu mkubwa ni hali hali yake ya kiafya, alibahatika sana kuwa hai baada ya kusafiri chini ya gurudumu la ndege kwa saa tano,'' alisema masemaji wa shirika hilo la ndege.

"huyu mtoto ana bahati sana kuwa hai,'' aliongeza kusema msemaji wa shirika la FBI.

Inaarifiwa punde tu baada ya ndege kutua, kijana huyo alishuka na kuanza kurandaranda katika uwanja wa ndege.

Kijana huyo alipatikana tu akiwa na kichana mkononi.

Aliponea sana, maana alikosa hewa huku akipigwa na baridi kali ndege ilipokuwa inaruka mita 12,000 juu angani.

Kadhalika kijana huyo anaarifiwa kupoteza fahamu muda wote wa safari.