Jeshi lawaokoa watu 10 kutoka kwa LRA

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jeshi la Uganda linashirikiana na wanajeshi wa AU kumsaka Joseph Kony

Jeshi la Uganda limesema kuwa limewaokoa watu 10 , saba kati yao wakiwa watoto, waliokuwa wametekwa nyara na wapiganaji wa kundi la waasi la LRA.

Watu hao waliokolewa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ambako kundi la LRA limekuwa likiendesha harakati zake kwa miaka mingi.

Msemaji wa jeshi la Uganda, amesema kuwa kamanda mmoja wa kundi hilo Charles Okello, alikamatwa pamoja na wapiganaji wengine wanne.

Marekani imekuwa ikisaidia wanajeshi wa Muungano wa Afrika wanaomsaka kiongozi wa kundi hilo Joseph Kony kwa kuwapa ushauri na kuwasaidia na ndege wanazotumia kumsaka kiongozi huyo.

Wanajeshi hao hawamsaki Kony tu anayetakikana na mahakama ya kimataifa ya jinai ICC, bali wanawatafuta na viongozi wengine wakuu wa kundi hilo