Madaktari 3 wa kigeni wauawa Afghanistan

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Madaktari wengine wawili wamejeruhiwa katika shambulizi hilo

Mlinzi mmoja nchini Afghanistan amewaua kwa kuwapiga risasi madaktari 3 raia wa Marekani wanaofanya kazi katika hospitali moja mjini Kabul.

Hosptali hiyo inayowahudumia watoto na kutoa huduma za afya ya uzazi inasimiwa na shirika la kikirsto la Marekani CURE.

Madaktari wengine wawili pia walijeruhiwa.

Mlinzi huyo kisha alijipiga risai na kwa sasa anazuiliwa na polisi.

Hili ndilo shambulizi la pili linalowalenga wakristo nchini Afghanistan mwaka huu.

Mwezi Machi wanamgambo wa Taliban walivamia jumba moja la kulala ambalo hutumiwa na raia wa kigeni wananaofanya kazi na shirika moja la kilimo.