21 wafariki nchini DRC Congo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanamke abubujikwa na machozi mbele ya mwili wa mwathiriwa wa kukanyagana nchini DRC Congo.

Takriban watu 21 wamefariki baada ya kukanyagana katika sherehe za muziki nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Maafisa wanasema kuwa tukio hilo lilifanyika katika tamasha ya mji wa kusini magharibi wa Kikwit ili kuadhimisha kifo cha mwanamuziki kester Emeneya ambaye alifariki mwezi uliopita.

karibia watu 12 walijeruhiwa.

Mashahidi wanasema kuwa umati wa watu ulikimbilia katika mlango wa kutokea kufuatia kukatika kwa umeme.

Uchunguzi kuhusu kisa hicho umeanzishwa.