Obama aionya korea kazkazini

Haki miliki ya picha AP
Image caption Korea kazkazini inayafanyia majaribio makombora yake.

Rais Barrack Obama wa Marekani amesema kuwa Korea Kazkazini imekubali kuchagua sera ya mapambano swala ambalo litapelekea jamii ya kimataifa kuzidi kulitenga taifa hilo.

Akiwahutubia wanajeshi wa marekani nchini korea kusini mwishoni mwa ziara yake katika taifa hilo,rais Obama alitofautisha kati demokrasia ilio korea kusini na kile alichokitaja kuwa uhuni unaondelea katika taifa la korea kazkazini ambalo amesema limechagua kuwakandamiza raia wake badala ya kuimarisha matumaini pamoja na ndoto zao.

Amesema kuwa hatua ya taifa hilo kutafuta silaha za kinuklia si ishara ya kuwa na uwezo na kwamba taifa hilo halitajipatia heshima kupitia kurusha kombora ama kulituma jeshi lake.

Rais Obama amewasili nchini Malaysia,ikiwa ni ziara yake ya tatu ya bara Asia.