Urusi kuingilia walioshikiliwa Ukraine

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanajeshi wa Ukraine

Jopo la ujumbe wa Urusi kwenye Shirika la ulinzi na Ushirikiano barani Ulaya wamesema watafanya kila njia kuhakikisha waangalizi wa kijeshi wa Umoja wa Ulaya walioshikiliwa mashariki mwa Ukraine wanaachiliwa huru.

Waangalizi wapatao wanane na Maafisa wengine wa kijeshi wa Ukraine walikamatwa hapo Ijumaa na wanaharakati wanaounga mkono Urusi katika mji wa Sloviansk.

Wapiganaji wa mji huo wanasema walioshikiliwa walikuwa wakituhumiwa kuwa walikuwa wakifanya upepelezi.

Kiongozi wa mji huo anayeunga mkono Urusi amesema waangalizi hao wangeachiwa kwa mpango wa kubadilishana wafungwa kwa wapiganaji waliokamatwa na majeshi ya Ukraine.

Waandishi kadhaa pia walikamatwa na kushikiliwa. Mwandishi wa BBC aliyeshikiliwa na kuachiliwa muda mchache baadaye, amesema mji huo hauna utawala wa kisheria na kuna wasi wasi nguvu za kijeshi zikatumika.

Marekani imesema ndege za kijeshi za Urusi zimeingia kwenye anga ya Ukraine mara kadhaa.