Kanisa lawataja wawili kuwa watakatifu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption papa francis

Katika sherehe iliofanyika katika mji wa Vatican,kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amewatangaza viongozi wawili wa zamani wa kanisa hilo john wa 23 na john paul wa pili kuwa watakatifu.

Mtangulizi wake papa Benedict amehudhuria hafla hiyo ambapo ni mara ya kwanza kwa viongozi wawili wa kanisa hilo kufanywa kuwa watakatifu.

Papa Francis amewataja watakatifu hao kama watu wajasiri walioweza kuliongoza kanisa hilo katika kipindi kigumu cha karne ya.

Amempongeza John wa 23 kwa uwazi wake wakati alipokuwa akilifanyia mabadiliko kanisa hilo.

Aidha kiongozi huyo amemtaja papa john wa pili kama kiongozi wa familia.

Maelfu ya mahujaji waliwasili katika mji huo, wengi wakiwa wametoka Poland, nchi ya john paul ambaye amefanywa kuwa mtakatifu miaka tisa tu baada ya kifo chake.

Bustani ya Saint Peters mjini Vatican ilijaa watu huku maafisa wakiwatafuta maaskari wa ziada ili kusimamia umati huo mkubwa.

Zaidi ya viongozi 20 wa mataifa tofauti wamehudhuria sherehe hiyo.