Wafuasi 11 wa Morsi wahukumiwa jela

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wafuasi wa aliyekuwa raia wa Misri Mohammed Morsi

Mahakama moja nchini Misri imewahukumu wafuasi 11 wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi kifungo cha kati ya miaka mitano hadi minane jela kwa kufanya maandamano.

Washtakiwa hao walikamatwa kufuatia msururu wa ghasia zilizozuka baada ya kundolewa madarakani kwa Mohammed Morsi mwaka uliopita.

Mnamo mwezi Machi, zaidi ya wafuasi 500 wa Mohammed Morsi walihukumiwa kifo katika mahakama hiyo hiyo.

kesi hiyo inajiri wakati ambapo kuna msako dhidi ya waislamu wenye itikadi kali wanaomuunga mkono Mohammed Morsi.