Afrika Kusini huru yatimiza miaka 20

Afrika Kusini ikisherehekea kutimiza miaka 20 ya uhuru Haki miliki ya picha AP

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amekuwa akiongoza sherehe za kutimiza miaka 20 ya demokrasi na kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi.

Akihutubia taifa Rais Zuma alisema Afrika Kusini inaanza kupona vidonda vya historia ya ukatili na mgawanyiko na taratibu inajenga umoja wa taifa.

Lakini alisema bado kuna kazi ya kukamilisha lengo la kuondosha umaskini, tofauti za pato na ukosefu wa ajira.

Sherehe hizo zinafanywa kabla ya uchaguzi mkuu ambapo chama tawala cha ANC kinakabili upinzani dhidi ya uongozi wa nchi tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka wa 1994.