Bouteflika aapishwa kwa muhula wa 4

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bouteflika alipiga kura akiwa kwenye kiti cha magurudumu

Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika ameapishwa kwa muhula mwingine wa miaka minne mamlakani katika hafla iliyofanyika mjini Algiers.

Vyombo vya habari vimeonyesha Bouteflika akiwa ameketi katika kiti cha magurudumu. Alionekana akiapishwa na kusema kwa sauti ya chini kuwa ushindi wake ni ushindi wa taifa zima.

Rais huyo ni mgonjwa na hata hakushiriki katika kempeini za kumchagua tena lakini licha ya hayo yote alishinda uchaguzi huo uliofanyika tarehe 17.

Bouteflika hajakuwa akionekana hadharani tangu apatwe na kiharusi mwaka jana huku maswali yakiibuka kuhusu uwezo wake wa kuliongoza taifa hilo.

Mwaka jana alilazwa hospitalini mjini Paris kwa miezi mitatu baada ya kupatwa na Kiharusi.