Mchunguzi wa Umoja wa Ulaya aachiliwa

Image caption Mchunguzi wa Umoja wa Ulaya aachiliwa huru

Mmoja wa wachunguzi wa muungano wa Ulaya waliokamatwa na wanamgambo wanaotaka kujitenga ambao wanaiunga mkono Urusi ameachiliwa huru katika mji wa Sloviansk nchini Ukraine.

Msemaji wa kundi hilo ameiambia BBC kwamba mwanamme huyo anayeaminika kuwa raia wa Sweden-aliachiliwa huru kwa misingi ya kiafya.

Mwangalizi huyo kutoka Sweden anayeaminika kuugua ugonjwa wa kisukari alionekana akisafirishwa kwa gari la Shirika la usalama na ushirikiano la mataifa ya Ulaya OSCE .

Lakini wenzake saba bado wanazuiliwa huku juhudi za kidplomasia kujaribu kuwakomboa zikiendelea.

Awali waangalizi hao walionyeshwa kupitia vyombo vya habari vya habari.

Mmoja wao ambaye ni Kanali kutoka Ujerumani , Axel Schneider, amesema waangalizi hao walikua katika harakati za kidiplomasia na hawakuwa na

silaha.

Shirila hilo la OSCE lina kundi kubwa la waangalizi nchini Ukraine ambao walikubaliwa na Urusi, lakini waangalizi hawa ni kutoka nchi kadhaa za

shirika hilo waliokwenda nchini Ukraine kwa mwaliko wa serikali.