Huwezi kusikiliza tena

Mabingwa Kenya waangushwa

Bingwa mtetezi Magereza ya Kenya imeshindwa seti 3-0 na GS Petroliers ya Algeria kwenye mechi ya fainali ya mashindano ya voliboli ya klabu bingwa Afrika nchini Tunisia.

Kenya Pipeline ilimaliza ya tatu kwa kushinda Carthage ya Tunisia seti 3-1.

Kwa matokeo hayo Magereza imepoteza taji lake na matumaini yao ya kushinda mara ya tano mfululizo kuzimwa.

GS Petroliers ilishinda seti ya kwanza 30-28, ya pili 25-15 na ya tatu 25-9..leo hii JN amezungumza kwa njia ya simu na maneja wa Magereza, David Kilundo, akiwa mjini Carthage, Tunisia...