Madereva wa treni wagoma Uingereza

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wasafiri waliokwama wakisubiri usafiri

Wasafiri nchini Uingereza wamekumbwa na changamoto ya usafiri baada ya wafanyakazi wa treni kugoma.

Chama cha wafanyakazi wa treni kimeanza mgomo wao wa siku mbili kutokana na mipango ya kufunga ofisi zote za kuu za tikiti za usafiri huku kukiwa na hofu ya watu 960 kupoteza ajira.

Halmashauri ya usafiri wa London, umesema kuwa ni kati ya asilimia 40 na 50 ya huduma za treni zitaweza kupatikana leo.

Mgomo huo ilianza Jumatatu usiku na utaisha Jumatano ingawa huenda bado kukawa na matatizo hadi siku ya Alhamisi.

Chama cha wafanyakazi pamoja na mnaafisa wa hamlashauri ya usafiri wa treni wamekutana zaidi ya mara 40 kuzungumzia tatizo hilo , lakini bado pande hizo mbili hazijaafikia lolote.

Wasafiri wameweza kupewa nyaraka kuhusu ushauri wa usafiri katika muda wote wa mgomo.

Usafiri mbadala utaweza kuwekwa kwa ajili ya kusaidia wasafiri hao , lakini wasafiri wameshauriwa kuwa waangalifu kuhusu ratiba yao ya usafiri kabla ya kusafiri.