Ronaldo avunja rekodi ya Messi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ronaldo avunja rekodi ya Messi

Nyota wa Real Madrid ya Uhispania Cristiano Ronaldo amevunja rekodi ya Lionel Messi ya ufungaji mabao mengi zaidi katika ligi ya mabingwa barani Uropa alipoifungia timu yake mabao mawili na kuisaidia

kuichapa Bayern Munich mabao 4-0 katika nusu fainali jana usiku.

Mreno huyo mwenye umri wa miaka , 29,alifunga bao lake la 15 na 16 msimu huu katika uwanja wa Allianz Arena.

Kufuatia ushindi huo Real Madrid ilifuzu kwa fainali ya mchuano huo kwa jumla ya mabao 5-0.

Ronaldo sasa amefunga mabao 16 katika mechi kumi za ligi hiyo ya mabingwa Barani Ulaya mbili zaidi ya Lionel Messi wa Barcelona .

Rekodi hiyo ya mabao 14 ilikuwa ikishikiliwa kwa pamoja kati ya Messi (2011-12, Barcelona), Ruud van Nistelrooy (2002-03, Manchester United) na Jose Altafini (1962-63, AC Milan).

Kwa jumla Ronaldo amefunga mabao 67 katika ligi hiyo ya mabingwa barani ulaya sawa na Messi na ni mabao manne tu nyuma ya rekodi ya idadio kubwa zaidi ya mabao yaliyofungwa na mchezaji wa zamani wa Real na Schalke Raul.