Raia wa DRC wafurushwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais kabila wa DRC Congo.

Mamlaka ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imesema kuwa takriban raia wake elfu sitini wamefurushwa kutoka taifa jirani la Congo- Brazaville katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

Congo -Brazaville inasema kuwa mpango huo ni miongoni mwa oparesheni kubwa za kuwafukuza wahamiaji haramu swala linalosababisha uhalifu.

Lakini waandishi wanasema kuwa ufukuzaji wa kiwango kama hicho si wa kawaida.

Serikali ya DRC imesema kuwa inachunguza madai ya unyanyasaji dhidi ya raia wake yaliotekelezwa na vikosi vya usalama nchini Congo-Brazaville.

Kuna ushirikiano mkubwa wa kibiashara na kikabila kati ya mataifa hayo mawili ambayo miji yake mikuu Kinshasa na Brazaville imegawanywa na mto Congo.

Meya wa Brazaville amesema kuwa afisa yeyote atakayepatikana akiwanyanyasa raia atafunguliwa mashtakiwa.