Mexico yadaiwa kuwatesa mahabusu

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Enrique Pena Nieto wa Mexico anayepunga mkono

Afisa mmoja mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amesema Mexico imekua ikiwatesa watuhumiwa inaowashikilia katika maeneo mbali mbali ya taasisi za serikali kuanzia jeshi, serikalini hadi jeshi la polisi.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mateso, Juan Mendez amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakiteswa wakati wa kukamatwa na hata wakati wa wakupelekwa mahakamani mbele ya majaji.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wa Mexico

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari amesema kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakipigwa ngumi, mateke, fimbo na kupigwa kwa shoti za umeme sehemu za siri.

Aidha Afisa huyo ameongezea kuwa mabadiliko katika sekta ya sheria kama vile kuwapatia mawakili wafungwa, kutapunguza mateso hayo.

Rais Enrique Pena Nieto amelipa kipau mbele swala hilo la kupunguza mateso hayo na kusema kuwa atatekeleza mapendekezo hayo.