Tahadhari kwa wezi wa simu mitaani

Image caption Mwizi aliyepigwa picha na simu hiyo ya HTC

Simu ya mkononi iliyokuwa imeibwa, ilituma ujumbe mfupi na picha ya mwizi wa simu hiyo kuonyesha kuwa ndiye mmiliki wake.

Polisi katika eneo la Essex nchini Uingereza wanamtafuta mwizi wa simu hiyo.

Simu hiyo aina ya HTC, iliibwa kutoka kwa koti la mwanafunzi mmoja alipokuwa safarini kuelekea nyumbani.

Mwenye simu alikuwa ameweka kifaa cha usalama kwenye simu hiyo ambacho kinaifanya simu kumpiga picha mtu anapojaribu kuingiza nambari ya siri au PIN mara tatu bila kufanikiwa.

Msemaji wa polisi alisema kuwa simu hiyo ilimpiga picha mwanamume huyo alipojaribu kuingiza nambari hiyo bila kufanikiwa.

Barua pepe ya mwanafunzi huyo ilituma ujumbe kwa polisi kuwaarifu kuhusu wizi huo.