Je Marekani imechelewa kusaidia Nigeria?

Haki miliki ya picha
Image caption Michele Obama emejiunga na kampeni hii kutaka kuachiliwa kwa wasichana wa Nigeria

Wiki tatu tangu wasichana zaidi ya miambili kutekwa nyara na Boko Haram nchini Nigeria, Jana ndio Marekani ilitangaza kutuma kikosi maalum kusaidia Nigeria kuwatafuta wasichana hao.

Je kimya hiki kilichukua muda mrefu kwa nini, jee kujihusisha kwa Marekani wakati huu kutasaidia hali?

Matukio machache yametendeka huku dunia nzima ikichukua muda kujibu mfano ikiwa hii taarifa ya kutekwa kwa wasichana wa Nigeria kutoka katika shule yao ya mabweni Kaskazini mwa Nigeria.

Maandamano yamefanyika mjini New York, Los Angeles na London,wakati ujumbe mwingi kupitia kwenye mitandao ya kijamii ikitolewa sio tu kwa Boko Haram bali pia kwa serikali ya Nigeria kwa kuonekana kama isioguswa na tukio hilo.

Mnamo siku ya Jumatano, mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama alituma ujumbe kwa Twitter uliosema 'BringBackOurGirls' yaani ''#Turudishieni wasichana wetu'' kuongeza sauti yake kwa kampeini ambayo imewaka moto dunia nzima.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ni wiki tatu tangu kutekwa nyara kwa wasichana wa Nigeria. Boko Haram imesema itawauza wasichana hao

Hii ni kamepin iliyoanza nchini Nigeria kuwataka Boko Haram kuwaaachilia wasichana hao.

Mchango wake kwa kampeini hii umekuja siku moja baada ya Marekani kutangaza kupeleka kikosi kusaidia Nigeria. Kikosi hicho kitasaidia Nigeria kwa upande wa uchunguzi, kuzungumza na wapiganajji kuwashawishi kuwaachilia wasichana na kuwasaidia waathiriwa.

Alipouliozwa kwa nini ilichukua mda mrefu, waziri wa mambo ya kigeni John kerry alijibu kuwa Marekani ilikuwa imejitolea kusaidia lakini serikali ya Nigeria ikawa haiko tayari kwa hilo.

"tumekuwa tukishauriana tangu tukio hilo kuripotiwa, lakini inaonekana serikali ya Nigeria ilikuwa na mikakati yake, '' alisema Kerry.

Lakini jibu hilo halijawakomesha watu kuuliza, kwa nini nchi za magharibi zimejikokota katika kusaidia Nigeria kama vile, Ufaransa, Uingereza na Marekani? Hata hivyo licha ya malalamiko haya msemaji wa serikali ya Uingereza amekanusha madai kuwa nchi hizo zimechelewa kusaidia Nigeria.

Baadhi ya wachanganuzi wamefananisha kuchelewa kwa mataifa hayo kusaidia Nigeria kinyume na ilivyokuwa wakati ndege ya Malaysia MH370 ilipopotea huku mataifa mengi tu yakijitolea kusaidia Malaysia.

Wakati mwingine bara la Afrika linaweza kuwa giza kuu kwa mataifa ya Magharibi , lakini sio kwa wakati huu ambapo msaada mkubwa unahitajika.