Riadha ya Diamond League kuanza leo Doha

Haki miliki ya picha
Image caption Usain Bolt anayetarajiwa kushiriki riadha ya Diamond League itakayokuwa Doha, Qatar.

Ni Mashindano ya Riadha yanayopambwa na wakimbiaji nyota duniani na huu ni mkondo wa kwanza.

Kuna jumla ya mikondo 14 ya mbio hizi ambazo zitamalizika tarehe tano Septemba mwaka huu mjini Brussels, Ubelgiji.

Mabingwa kama vile Usain Bolt , Yohan Blake huwa vivutio vikubwa lakini muhimu zaidi mashindano hayo ni jukwaa mojawapo kubwa la kuonyesha nyota wa Afrika mashariki na kati.

Miongoni mwa wanaotarajiwa kupeperusha bendera ya Afrika kama kawaida ni wa-Ethiopia kama vile Mohamed Aman na wakenya , akina Job Kinyor, Kipkorir Mutahi wanatarajiwa kumpa upinzani mkali Nijel Amos mshindi wa medali ya fedha mbio mita 800 katika olympiki iliyopita ya London kwani bingwa David Rudisha mkenya huenda asishiriki kwa sababu angali anauguza jeraha.

Katika mbio kama zile za mita 3000 kuruka viunzi, wake kwa waume wakenya hufanya vizuri lakini ushindani ni mkubwa.