Ferdinand kuondoka Old Trafford

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ferdinand kuhama Old Trafford

Mlinzi wa Manchester United Rio Ferdinand amesema ataondoka Old trafford msimu ujao baada ya klabu hiyo kukataa kumuongezea muda kwenye kandarasi yake.

Kauli hiyo inamaanisha Ferdinand ambaye amefunga mabao nane Old Trafford katika miaka 12 na kushiriki katika mechi 454 ataingia katika orodha ndefu ya wachezaji wakongwe mabalozi wa klabu hiyo.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa mlinzi huyo anapania kuendelea kucheza lakini haijulikani ataichezea klabu ipi.

Ferdinand alisema katika barua ya wazi kwa klabu hiyo kuwa angelipenda kuwaaaga mashabiki wake kwa njia bora zaidi lakini kutokana na ati ati hangeweza . Hata hivyo amesema kuwa amefikiria sana kuhusu hatima yake na umewadia wakati wake kuwaaga.

Ferdinand aliwasili United Agosti 2002 kutokea klabu ya Leeds timu hiyo ilipokuwaikikabiliana na Hungary Zalaegerszeg katika mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Ameshinda mataji 6 ya ligi kuu ya premia mbali na mataji mawili ya nyumbani .

Manchester Utd pia ilishinda taji la klabu bingwa duniani mbali na taji la mabingwa barani Uropa.