Justin Bierber achunguzwa kwa kosa la wizi

Image caption Bierber akiwa jukwaani

Mwanamuziki wa kimataifa wa mtindo wa Pop Justin Bieber anachunguzwa na polisi kwa madai ya wizi

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 20, ambaye bado hajakamatwa, alituhumiwa kwa kosa la kuumuibia mwanamke mmoja shabiki wake.

Kulingana na mtandao wa taarifa za wasanii wa kimataifa, TMZ, Bieber anatuhumiwa kumnyang'anya mwanamke huyo simu yake.

Inaarifiwa mwanamke huyo alikua ametumia simu yake kumpiga picha Bieber lakini pindi aliporudisha simu yake kwenye kibeti chake, Bieber naye akaiiba simu hiyo katika uwanja wa kuchezea Golf mjini Los Angeles.

Kufikia sasa hakuna mtu aliyekamatwa na polisi wanamhoji mwanamke anayeyei kubiwa simu yake na Bieber.

Mwanamuziki huyo amekuwa akikumbwa na matatizo ya kujitakia tangu mwanzoni mwa mwaka huu mwanzo kwa kuendesha gari akiwa mlevi mjini Miami.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Bieber akiwatumbuiza mashabiki.

Kesi kuhusu tukio hilo inatarajiwa kusikilizwa mwezi Julai.

Polisi mjini California pia wamefanya msako kwa nyumba yake baada ya Bieber kudaiwa kurusha mayai kwa nyumba ya jirani wake.

Wiki tatu zilizopita, Bieber alizuiliwa na polisi katika uwanja wa kimataifa wa ndege na kuhojiwa na maafisa wa ushuru baada ya kurejea kutoka barani Asia.

Hata hivyo,hakuna hatua iliyochukuliwa na polisi kwani walimwachilia tu baada ya saa nne.

Bila shaka visa hivi vimemharibia sifa mwanamuziki huyo. Alizomewa aliposhinda tuzo ya vijana ya Juno Awards mwezi jana nchini Canada alikozaliwa.

Jumapili pia alizomewa kwa mara nyingine alipokwenda na mamake katika mchuano wa Basketball mjini Los Angeles.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii