ICC:Mwanahabari wa Kenya kukamatwa

Mahakama kuu nchini Kenya imetoa kibali cha kukamatwa kwa mwandishi wa habari Walter Barasaambaye atakabidhiwa kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.

Barasa anatuhumiwa kwa kuwashawishi mashahidi wa mahakama ya kimataifa ya ICC katika kesi inayomkabili naibu Rais William Ruto kutotoa ushahidi wao.

Bwana Ruto yuko katika mahakama hiyo ya The Hague mwenyewe akikabiliwa na madai ya kukiuka haki za binadamu wakati wa ghasia za baada ya uchguzi mkuu mwaka 2007.

Mnamo mwezi Machi, mahakama kuu iliamua kuwa bwana Barasa anaweza kupelekwa Hague akajibu mashitaka.

Anadaiwa kuwapa hongo mashahidi wa upande wa mashitaka , madai ambayo Barasa amekanusha.

Naibu Rais Ruto na mshitakiwa meingine Joshua Arap Sang wako katika mahakama ya ICC kujibu tuhuma za kufanya uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Wanadiwa kuchochea ghasia kwa misngi ya ukabila madai ambayo watuhumiwa wamekanusha. Pamoja nao mshitakiwa mwingine ni Rais Uhuru Kenyatta ambaye kesi yake iliahirishwa hadi baadaye mwakani.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii