Wandishi wa Al-Jazeera wanyimwa dhamana

Image caption Wandishi wa Al Jazeera wanaozuiliwa Misri

Kesi dhidi ya wandishi watatu wa habari wa shirika la habari la Al-Jazeera, imeahirishwa kwa wiki nyingine moja na washitakiwa kunyimwa dhamana tena

Wandishi hao wanatuhumiwa kwa kueneza habari potovu na kulisaidia vuguvugu la Muslim Brorherhood, lililoharamishwa na serikali.

Wandishi hao ni pamoja na Mohamed Fahmy aliyekuwa mhariri mkuu katika ofisi ya shirika hilo mjini Cairo, aliyeuwa mwandishi wa BBC Peter Greste pamoja na Baher Mohamed.

Wamekuwa wakizuiliwa tangu Disemba mwaka jana.

Mwandishi mwingine wa nne Abdullah al-Shami, amekuwa akizuiliwa tangu Agosti mwaka jana ingawa hajafunguliwa mashitaka.

Amekuwa akisusia chakula kwa siku 100 akipinga kuzuiliwa kwake.