BJP yaongoza katika Uchaguzi India

Image caption Chama cha BJP kinaongoza katika matokeo ya awali

Shughuli ya kuhesabu kura imeanza rasmi nchini India baada ya uchaguzi uliodumu kwa kipindi cha wiki tano.

Matokeo ya awali yanaashiria ushindi kwa muungano unaoongozwa na mgombea wa upinzani Narendra Modi aliayeahidi nafasi za ajira na maendeelo ya kiuchumi.

Kuna hali ya shangwe kwenye makao makuu ya chake cha BJP mjini Delhi kulikowekwa televisheni kubwa zinazoonyesha matokeo huku pia nyimbo zikiimbwa.

Hata hivyo utulizu umeshuhudiwa kwenye makao makuu ya chama tawala cha Congress.

Kiongoi kutoka kwa chama cha Congres Abhishek Manu Singhvi anasema kuwa matokeo yalioneka yasiyo na matumaini akiongeza kuwa hayo ndiyo matokeo mabaya zaidi kuwai kushuhudiwa na chama hicho.

Zaidi ya watu milioni mia tano walipiga kura na kuweka rekodi mpya wa wapiga kura ku asilimia sitini na sita.