Mali:Je ndege ni muhimu kuliko maendeleo?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Catherene Samba Panza rais wa kwanza mwanamke wa Mali

Serikali ya Mali imepuuza mzozo unaotokota kati yake na shirika la fedha duniani IMF kuhusu hatua ya kumnunulia Rais wa nchi hiyo ndege kuu kuu kwa kima cha dola milioni arubaini, hata baada ya kuahidi kulipatia swala la umasikini kipaombele.

Maafisa wa Mali watahojiwa hii leo katika mkutano wa wafadhili hao wa kimataifa.

Shirika la fedha Duniani I-M-F ndilo lilihoji kwa nini ununuzi wa ndege hiyo ulifanyika wakati nchi hiyo ina mambo mengi muhimu ya kushughulikia kuliko kumnunulia Rais ndege iliyozeeka.

Mwakilishi wa IMF nchini Mali, Anton Op de Beke, aliambia BBC kuwa hawajaelezwa kikamilifu kwa nini serikali ilifanya hivyo.

Lakini waziri wa mawasiliano wa nchi hiyo ,Mamadou Camara, alisema kuwa walikuwa wameieleza serikali kuhusu mpango wa kununua ndege hiyo na kuwa nchi hiyo ina uhusiano mzuri tu na shirika la IMF.

Wahisani wa kimataifa, ambao wako nchini Mali, wanatarajiwa kuhoji ununuzi huo pamoja na kandarasi ya ulinzi iliyotolewa na nchi hiyo na ambayo itaigharimu serikali dola milioni miambili.

Mwaka mmoja uliopita , wahisani waliahidi kuipa Mali dola bilioni nne kuisaidia serikali kukarabati nchi baada ya vita.