Waandishi waachiliwa Syria na wapiganaji

Mwandishi wa habari na mpiga picha wanaofanya kazi na gazeti la Times wameachiliwa baada ya kutekwa nyara na kundi la waasi nchini Syria.

Wote wawili, Anthony Lyod na Jack Hill, ambao wana ujuzi wa muda mrefu wa kuandika na kupiga picha za habari, walikuwa wakirudi kutoka eneo la Aleppo, Syria, walipotekwa nyara na kundi la wapiganaji karibu na mpaka wa Uturuki.

Bwana Hill alijaribu kutoroka lakini alikamatwa na kupigwa vibaya.

Bwana Lyod pia alipigwa risasi miguuni mara mbili kumzuia kutoroka na pia akapigwa vibaya.

Waandishi hao wa habari walisema kuwa waliachiliwa baada ya kuingilia kwa kundi kubwa la waasi nchini Syria la, Islamic Front.