10 wauawa katika milipuko Nairobi

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Haijulikani na nani aliyesababisha milipuko ingawa washukiwa tayari wamekamatwa

Milipuko miwili ilitikisa Soko kubwa la nguo la Gikomba mjini Nairobi na kuwaua watu 10 huku zaidi ya hamsini wakijeruhiwa..

Soko hilo linapakana na mtaa wa Easleigh ambako wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.

Shirika la serikali la kushughulikia majanga linasema kuwa angalau watu 10 wamefariki na wengine zaidi ya hamsini kujeruhiwa.

Mlipuko wa kwanza ulitokea katika gari la abiria wakati la pili likitokea ndani ya soko.

Image caption Soko la Gikomba ni maarufu kwa nguo za mitumba

Milipuko hiyo ilitokea siku moja baada ya Uingereza kutoa onyo kwa raia wake wanaoishi nchini humo kurejea makwao kwa hofu ya usalama na pia baada ya tahadhari kutolewa ya kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi nchini humo.

Gikombaa ni soko kubwa la kuuza nguo ambalo linapakana na mtaa wa Eastleigh ambako wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.

Kenya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa wawu wenye uhusiano na kundi la wanamgambo la kiisilamu nchini Somalia la Al Shabaab.

Polisi wamewakamata washukiwa wawili.