Modi apongezwa kwa ushindi India

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Narendra Modi akiwasalimia wafuasi wake

Mtu anayetarajiwa kushika wadhifa wa Waziri Mkuu nchini India Narendra Modi amepongezwa na umati mkubwa wa wafuasi wake mjini Delhi baada ya chama chake cha BJP kuibuka mshindi katika uchaguzi mkuu nchini humo.

Bwana Modi ambaye amepanda kutoka kuwa muuza chai hadi kuwa kiongozi wa watu billioni moja amekutana na viongozi wa juu wa chama chake cha BJP katika makao makuu ya chama hicho baada msafara wa maandamano ya kumpongeza kutoka uwanja wa ndege.

Image caption Wafuasi wa Narendra Modi

Maelfu ya raia waliokuwa wakipeperusha bendera za BJP na kuimba wimbo wa kumsifu walijipanga kando kando ya barabara aliyokuwa akipita kwa lengo la kumpongeza kwa ushindi.

Mapema hii leo, Waziri Mkuu anayemaliza muda wake, Manmohan Singh aliwasilisha barua yake ya kujizulu kwa rais Pranab Mukherjee.

Katika hotuba yake ya mwisho kwa njia ya televisheni Bwana Singh amesema India imekuwa nchi imara zaidi kuliko ilivyokuwa mionogo kadhaa iliyopita wakati alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu.