Watu 70 wauawa katika vita nchini Libya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanamgambo nchini Libya

Maafisa nchini Libya wanasema kuwa idadi ya watu waliofariki katika vita mjini Benghazi imeongezeka na kufikia zaidi ya 70.

Jeshi limetangaza kwamba hakuna ndege itakayoruhusiwa kupaa juu ya mji huo huku spika wa bunge akisema kuwa mtu anayeongoza vita hivyo Khalifa Haftar anajaribu kufanya mapinduzi.

Bwana Haftar amesema kuwa ataendelea na kampeni yake ya kuwaondoa wale aliowataja kama magaidi nje ya mji wa Benghazi huku akiongezea kuwa anaungwa mkono na raia wengi wa mji huo ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Libya.

Hatahivyo familia nyingi zinahamia magharibi mwa mji huo kufuatia vita vikali kati ya vikosi vya Haftar na wanamgambo.