Umasikini kikwazo cha kulea watoto China

Image caption Wazazi wa Miaomiao walikuwa na wakati mgumu kuamua ikiwa wamkbadhi mwanao kwa serikali au kumtupa

Wakati Liu Jiaomei alipojifungua mwanawe wa kike, Miaomiao mnamo mwezi Machi, alilazimika kuondoka hospitalini saa moja baada ya kujifungua.

Bi Liu na mumewe wote wakiwa wafanyakazi wahamiaji, hawakuwa na pesa za kutosha kulipia huduma zaidi za hopsitalini.

Liu na mumewe wakampeleka mtoto wao hospitalini lakini walijua kuwa mtoto huyo alikuwa mgonjwa sana.

Miaomiao anaumwa sana na miguu yake. Ana shimo kubwa mdomoni mwake na hivyo hupata matatizo kumeza chakula. Ana miezi sita sasa na uzani wake umeanza kupungua.

"nilitaka kumchunga mtoto wangu mimi mwenyewe,'' alisema Liu Jiaomei, akibubujikwa na machozi. Lakini mume wangu akaniuliza , itakuwaje mtoto wetu akifariki kwa sababu tumeshindwa kumpa malezi mazuri,''?

'Maisha magumu'

Bila pesa na huduma za afya kutoka kwa serikali, wazazi hawa wanakumbwa na wakati mgumu kutoa uamuzi mgumu kuhusu mtoto wao. Ima wamkabidhi kwa serikali ambako atapata malezi mazuri au waendelee kuishi naye wakisubiri afe.

"hakuna anayetaka kumtupa mwanawe,'' asema babake Miaomiao, Lei Zebao.

"lakini ikiwa tutamkabidhi kwa serikali, tunadhani atakuwa na nafasi nzuri ya kupona. ''

Wazazi wa Miaomiao wanaishi katika mkoa wa Guangzhou ambako wanakumbwa na hali ngumu ya kiuchumi.

Image caption Lei Zebao (Kushoto) na Liu Jiaomei (Kulia) wanaishi kwa umaskini mkubwa

Hatimaye waliamua kumpeleka mtoto wao katika makao salama ya watoto ambayo iko karibu na nyumbani kwao.

'Afya ya uzazi china'

Baadhi wanasema kuwa China imepiga hatua kubwa katika kufanikisha afya ya uzazi kwa wanawake wengi nchini humo...Mgala muue lakini haki yake mpe.

Kiwango cha wanawake kufariki kutokana na matatizo ya uzazi kimepungua nchini China kwa zaidi ya asilimia 13. Shirika la afya duniai linatambui hilo.

Lakini idadi hii haina maana kubwa kwa familia masikini ambazo zinakabiliwa na wakati mgumu kuwalea watoto wao, hasa kwa kuwa kipato chao ni cha chini mno.

Serikali ya China imeweka vituo kadhaa kando ya barabara ambako wazazi huwaacha watoto wao ambao baadaye wanachukuliwa na maafisa wa serikali

Tarehe 16 mwezi Machi, wazazi hao walifunga safari wakiwa wamemfunika mtoto wao vyema kumpeleka katika moja ya vituo hivyo.

Hata hivyo makao hayo yalikuwa hayawapokei watoto tena hasa kwa kuwa wale ambao tayari wako katika makao hayo ni wgaonjwa sana, lakini kwa bahati nzuri mtoto Miaomiao alweza kuchukuliwa.

Image caption Sehemu ambapo wazazi wanaruhusiwa kuwaacha watoto wao wanaochukuliwa na serikali

Yaliyofunguliwa mwezi Januari ili kuwapa wazazi wasiojiweza mahala pa kuwaacha watoto wao bila ya watu kujua.

"nilikuwa naomba kimya kimya kua wasimchukue mtoto wangu, lakini sikuwa na uhakika kama ninaweza kumtunza vyema, '' ulikuwa wakati mgumu kwangu,'' alisema mamake Miaomiao ambaye anaishi katika chumba cha kutengeza magari karibu na barabara.

Hawana uwezo wa kununua maziwa na nepi za mtoto, Changamoto za kujikimu ni nyingi kwao.

Mnamo mwezi Machi, makao ya kuwahifadhi watoto ya Guangzhou, yalifungwa lakini baada ya malalamiko , yalifunguliwa baada ya wiki sita ......Watoto watano walipokelewa siku hiyo hiyo.

Kwa jumla watoto 262, walikuwa wamekabidhiwa kwa serikali. Wote walikuwa na matatizo ya kiafya ikiwemo magonjwa ya moyo na ya uti wa mgongo.

'Je makao ya watoto ni wazo zuri?'

Image caption Mmoja wa watoto walioachwa katika kituo cha kuwahifadhi watoto walioachwa na wazazi wao

Serikali ya China imeamua kufungua makao zaidi katika miji mingine mikubwa nchini humo.

Ni kinyume na sheria kumtupa mtoto wako nchini China, lakini makao hayo ya kuwahifadhi watoto, yanawapa nafasi wazazi wasioweza kuwalea watoto wao, kuwapeleka watoto wao katika makao hayo bila ya kujulikana na pia bila ya kupata adhabu yoyote.

Lakini sio kila mtu anapenda wazo hili.

Shirika moja la kutetea haki za watoto nchin Uingereza la Lumos, linasema makao ya kuwahifadhi watoto wasiotakikana na wazazi wao lazima yafungwe.

Hata hivyo maafisa wa China wametetea vikali umuhimu wa makaazi ya kuwalea watoto waliotupwa na wazazi wao wakisema kuwa watoto wanaotupwa kwenye barabara za mji wana fursa ya asilimia 30 pekee kuishi lakini wale wanaohifadhiwa wanaweza kupona na kuishi maisha marefu.