Watu 17 wauawa nchini Mali

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri mkuu wa Mali Muossa Mara

Kuna hali ya wasiwasi mjini Kidal Kaskazini mwa Mali ambapo takriban watu 17 wameuawa katika mapigano ya siku tatu.

Waasi wa kundi la Tuareg wamewakamata wanajeshi 28 pamoja na raia.

Jeshi la Mali limetuma wanajeshi zaidi huku waziri mkuu nchini humo akitangaza vita.

Wakaazi wa mji wa kidal wameiambia BBC kwamba wanaogopa baada ya kusikia ripoti kutoka kwa redio ya taifa hilo kwamba waziri mkuu Mousa Mara ametangaza vita.

Baadhi yao wameanza kubeba vitanda wakitoroka eneo hilo huku kukiwa na hofu ya kwamba jeshi la Mali linajiandaa kutekeleza mashambulizi.

Waasi wa AZAWAD wamekiri kuwakamata watu 28 baada ya ziara ya waziri mkuu katika eneo hilo Jumamosi iliopita.

Serikali imewashutumu waasi hao kwa kuwaua raia 8,lakini waasi hao wanadai kuwa wanane hao waliuawa kufuatia ufyatulianaji wa risasi.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii