Rais Morales kucheza kiungo cha kati

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Morales ni shabiki sugu wa kandanda

Hebu tafakari rais wa nchi kuchezea klabu ya kandanda inayoshiriki ligi ya taifa ya daraja la kwanza ?

Klabu moja huko Bolivia (Sport Boys) imemsajili rais wa Bolivia Evo Morales kucheza kama kiungo cha kati kuanzia Agosti mwaka huu.

Rais Morales atalipwa mshahara wa dola $213 kwa mwezi .

Morales atavalia jezi nambari 10 katika klabu hiyo iliyoko Kusini mwa Bolivia katika jimbo la Santa Cruz.

Mashabiki wanamsubiri kwa udi na uvumba kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 54 ambaye ni shabiki sugu wa kandanda kushuka dimbani.

Rais huyo ambaye ni shabiki sugu wa kandanda na mwenye umri wa miaka 54 ataichezea Sports Boys, timu ilyoko kusini mashariki mwa mkoa wa Santa Cruz.

Timu hiyo iliyoko katika ligi ndogo ilisema kuwa rais huyo atakuwa akicheza angaa kwa dakika 20 katika kila mchuano, hasa ikizingatiwa kuwa ni mtu mwenye shughuli nyingi.

Rais wa klabu hiyo alisema kwamba rais huyo anapenda kandanda, na kwamba yeye hucheza vizuri.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Evo Morales akiwa uwanjani

‘’Tutamtumia orodha ya michuano, kisha atachagua michuano anayotaka kushiriki,” alisema rais huyo.

Edwin Tupa, mwanasiasa kutoka katika chama cha MAS, ambacho ndicho chama tawala nchini humo, alisema kuwa ndoto ya rais huyo ya kuchezea klabu ya kiitaaluma ilikuwa imetimia.

Inasemekana kuwa rais huyo yuko sawa na ni mwenye furaha katika matarajio yake ya kucheza kandanda.

Bwana Morales amewahi kucheza katika mechi nyingi iliyotambulika pamoja na wanahabari, viongozi wa umoja na marais wengine.

Mwaka wa 2007, rais huyo alishiriki katika mechi iliyokusudiwa kupinga kikwazo kilichokuwa kimewekewa Bolivia, cha kutoshiriki katika mechi za kimataifa katika sehemu zenye urefu.

Mwaka wa 2006, alivunjika pia alipogongana na mlinda lango.