Pistorius kufanyiwa uchunguzi wa akili

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Pistorius akiwa mahakamani

Jaji katika kesi inayomkabili Oscar Pistorius anasema kuwa mwanariadha huyo lazima aanza kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kuanzia Jumatatu wiki ijayo kwa mwezi mmoja kubaini hali ya akili yake alipomuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Jaji Thokozile Masipa aliamuamuru Pistorius kua awe anakwenda katika hospitali ya maradhi ya kiakili ya Weskoppies mjini Pretoria kila siku kuanzia tarehe 26 mwezi Mei.

Amri ya jaji inakuja baada ya shahidi mmoja wa upande wa mashitaka kusema kuwa mwanariadha huyo anakumbwa na matatizo ya kuzongwa na mawazo pamoja na kuwa na wasiwasi wakati wote

Bwana Pistorius amekanusha madai ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kusudi

Anasema kwamba kwa bahati mbaya alimpiga risasi kupitia mlango wa choo baada ya kushikwa na wasiwasi akidhani kuwa alikuwa jambazo aliyevamia nyumba yake.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii