McIlroy avunja uchumba na Wozniacki.

Image caption Mchezaji gofu Rory McIlroy amevunja uchumba na mchezaji tenis Caroline Wozniacki.

Mchezaji gofu nambari kumi duniani Rory McIlroy amevunjilia mbali mipango ya harusi yake na aliyekuwa mchezaji tenis nambari moja duniani Caroline Wozniacki.

Raiya huyo wa Ireland ambaye ni bingwa wa mataji mawili ya gofu duniani amewaambia waandishi wa habari kuwa aligutushwa na kadi za mwaliko wa harusi yake na akang'mua kuwa hayuko tayari kwa majukumu ya ndoa

McIlroy na binti huyo kutoka Denmark, Wozniacki, walitangaza kuchumbiana januari mosi mwaka huu lakini kutokana na taarifa hiyo inaonekana uchumba wao wa miaka mitatu sasa umefikia kikomo.

McIlroy alisema hakuna njia bora ya kuvunja uhusiano baina ya wachumba lakini mimi ninamtakia kheri Wozniacki katika maazimio yake ya baadaye.

Image caption Mchezaji gofu Rory McIlroy amevunja uchumba na mchezaji tenis Caroline Wozniacki.

Mchezaji gofu huyo alisema kuwa kosa ni lake wala sio la Wozniacki .

McIlroy ambaye anajiandaa kwa mchuano wa 'The BMW PGA Wentworth utakaoanza hapo kesho nchini Uingereza ,amesema kuwa atajitahidi kumakinikia mchuano huu kwani sasa mambo ya uchumba yamepita.

Wozniacki, kwa upande wake anajiandaa kwa mchuano wa tenis ya wazi ya Ufaransa utakaonza tarehe 25 mwezi huu .

Wachanganuzi wa maswala ya mahusiano baina ya wachezaji wenye ushabiki mkubwa wanasema kuachana kwa nyota hao wawili imekuwa ghafla kwani majuzi (jumapili) McIlroy alichapisha picha yao wawili wakila chajio katika mkahawa mooja wa kifahari mjini Monte Carlo.

Wawili hao waliopewa jina la utani la pamoja la 'Wozilroy' waliwaduwaza mashabiki wao walipoanza usuhuba mwaka wa 2011 baada ya kukutana katika mechi ya masumbwi.