Nepal yawaagiza polisi wake kutabasamu

Image caption Polisi watakiwa kutabasamu Nepal

Je wamkumbuka koplo wa polisi nchini Kenya ambaye alizua mjadala Afrika Mashariki na Kati kwa jinsi aliyovalia sketi iliyombana makalio ? Sasa polisi nchini Nepal wameagizwa kuwa wapole na wenye tabasamu haswa wanapotangamana na raiya wa taifa hilo.

Msemaji wa Polisi nchini Nepal amesema kuwa serikali ya taifa imewatuma wakufunzi 600 wa maswala ya tabia na uhusiano mwema katika majimbo yote nchini humo kujaribu kuboresha uhusiano baina ya maafisa wa polisi na umma.

Image caption Polisi watakiwa kutabasamu Nepal

Kampeini hiyo imepewa jina la "huduma na tabasamu"na inanuiwa kufuta kumbukumbu ya uhusiano baina ya polisi na umma wakati wa vita vya wenyewe kwa wenye nchini humo.

Msemaji wa polisi KC Ganesh amesema kuwa maafisa 67,000 katika wilaya 75 ya Nepal wamelengwa katika kampeini hiyo mpya.