Urusi na Uchina zasaini mkataba wa gesi

Rais Vradimir Putin(kushoto) na Rais Xi Jinping(kulia) Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Rais wa Urusi Vradimir Putin akisalimiana na mwenzake wa Uchina Xi Jinping

Urusi imekubali kuipatia Uchina gesi , kufuatia mkataba wa mabilioni ya dola ambao mataifa hayo mawili yamekuwa yakiujadili kwa kipindi cha muongo mmoja .

Mkataba huo unadhaniwa kuwa wenye thamani ya dola bilioni mia nne na utadumu kwa zaidi ya miaka thelathini.

Wachambuzi wanasema kuwa matatizo ya kisiasa ya Urusi na mataifa ya magharibi kuhusu mzozo unaoendelea nchini Ukraine, yameisukuma Urusi kukamilisha mkataba huo na Uchina, ili kupata soko la rasilimali yake.

Mapatano hayo yamesainiwa katika sherehe zilizofanyika mjini Shanghai na kuhudhuriwa na rais wa Uchina , Xi Jinping, na mwenzake wa Urusi , Vladimir Putin.