Rais Zuma kuapishwa kwa muhula wa 2

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Jacob Zuma

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ataapishwa hii leo kwa muhula wake wa pili baada ya kushinda uchaguzi mkuu.

Chama tawala ANC, kilipatwa ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 7 mwezi Mei.

Zaidi ya wageni 4,000 mashuhuri wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo akiwemo Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.

Marekani na Uingereza hazitawakilishwa lakini maafisa kutoka Urusi, China na India watahudhuria hafla hiyo.

Rais Zuma alichaguliwa rasmi kwa muhula wa pili wa miaka mitano huku akipata bunge lenye waakilishi wengi wa bunge wa chama cha ANC.

Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa sherehe za kuapishwa kwa Zuma zitakuwa pia za kusherehekea miaka 20 ya demokrasia na kumbukumbu kwa Rais wa kwanza mzalendo wa nchi hiyo hayati Nelson Mandela

Marais wengine watakaohudhuria sherehe hizo ni pamoja na Goodluck Jonathan wa Nigeria na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii