Watatu wauawa na mlipuko nchini Nigeria

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Gari lilolukuwa na mlipuaji wa kujitolea muhanga mjini Jos.

Maafisa wa polisi nchini Nigeria wanasema kuwa watu watatu wameuawa baada ya mtu wa kujitolea muhanga kujilipua katika mji ulio katikati ya Nigeria Jos.

Mlipuko huo ulitokea karibu na eneo ambalo mashabiki wa soka walikuwa wakiangalia kinyanganyiro cha fainali za kombe la kilabu bingwa barani ulaya.

Ripoti zinasema kuwa mlipuaji huyo alikuwa amelilenga eneo hilo,lakini gari lake likalipuka kabla ya kufika.

Shambulizi hilo linajiri siku kadhaa tu baada ya takriban watu 118 kupoteza maisha yao katika milipuko miwili ya mabomu yaliotegwa ndani ya gari katika mji huo.