Wayahudi wapewa usalama Ubelgiji

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Maafisa wa polisi wawasili katika eneo la mashambulizi ya Wayahudi mjini Brussels,

Mamlaka nchini Ubelgiji imeimarisha usalama katika makaazi ya wayahudi baada ya mtu aliyejihami kwa bunduki kufyatua risasi katika makavazi ya wayahudi katika mji mkuu wa Brussels na kuwauwa watu watatu na kumjeruhi vibaya mtu mmoja.

Wazir mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekishtumu kitendo hicho na kukitaja kuwa cha uchochezi dhidi ya raia wa kiyahudi na taifa lao.

Maafisa wa Polisi wa Ubelgiji wamesema kuwa wamemkamata mtu mmoja aliyetoroka eneo hilo na wanamsaka mtu mwengine.