Makundi yenye itikadi kali yavunjwa China

Haki miliki ya picha
Image caption Kikosi maalum cha polisi tayari kwa mapambano na wanaozua vurugu

Vyombo vya habari nchini China vimeripoti kwamba maafisa wa polisi wameyavunja makundi 23 yenye itikadi kali na kuwakamata zaidi ya washukiwa 200 mwezi huu katika jimbo la Magharibi la shinjiang.

Tangazo hilo linafuatia shambulizi kali katika mji mkuu wa jimbo la Umruq lililosababisha mauaji ya watu 30.

China imewalaumu waislamu wenye itikadi kali kutoka jimbo hilo kwa misururu ya mashambulizi.

Kulingana na ripoti za vyombo rasmi vya habari maafisa wa polisi walitekeleza misako iliowanasa watu kadhaa na kukamata vilipuzi kadhaa.

Xhinua imeripoti kwamba idadi kubwa ya watu waliokamatwa wanatoka katika kundi la jamii ya waislamu walio wachache wa Uighur ambao wana ujuzi wa kutengeza vilipuzi kupitia kanda za video katika mtandao.

Pia imeshtumu washukiwa hao kwa kueneza ujumbe wa jihad kupitia mitandao ya kijamii.

Beijing imewalaumu watu wanaotaka kujitenga wa jamii ya Uighur kwa misururu ya mashambulizi katika maeneo mbali mbali nchini humo.

Lakini watu wa jamii ya Uighur walio mafichoni wamesema kuwa ghasia hizo zinachochewa na ukandamizaji wa dini na utamaduni wa Uighur unaofanywa na serikali.