Wachezaji 2 wa Ujerumani katika ajali

Image caption Wachezaji 2 wa Ujerumani wajeruhiwa Italia

Wachezaji wawili wa timu ya taifa ya Ujerumani itakayoshiriki kombe la dunia hukop Brazil mwezi ujao wamenusurika baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wakiwa Italia.

Benedikt Hoewedes na Julian Draxler walikuwa ndani ya magari tofauti katika hafla iliyoandaliwa na kampuni ya magari ya Mercedes .

Moja ya magari yaliyohusika iliwagonga wapita njia wawili karibu na makahawa wanakoiswahi timu ya taifa ya Ujerumani.

Mwathiriwa moja anauguza majeraha mabaya .

Image caption Wachezaji 2 wa Ujerumani wajeruhiwa Italia

Ajali ya pili ilimhusisha dereva wa mbio za magari ya langalanga wa Mercedes , Nico Rosberg.

Hoewedes na Draxler ni wachezaji wa timu ya Schalke 04 walioitwa katika timu ya taifa.

Wenyeji wao kampuni ya Mercedes-Benz imetoa taarifa kusema kuwa itashirikiana na maafisa wa polisi kutathmini kilichotokea .

Timu hiyo ya Ujerumani inatarajiwa kuendelea na kambi ya mazoezi katika mji wa Tyrol Kusini mwa Italia hadi juni mosi. .