Kura kupigwa kwa siku ya 3 Misri

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Idadi ya waliojitokeza kupiga kura ilikuwa chini ya matarajio ya tume ya uchaguzi

Vituo vya kupigia kura vimefungua kwa siku ya tatu nchini Misri, ambako wapiga kura wanamchagua Rais mpya.

Uchaguzi huo ulipaswa kufanyika kwa siku mbili , lakini umeongezwa muda ili kutoa fursa kwa wapiga kura zaidi kwenda kupiga kura.

Duru zinasema kuwa idadi ya watu walijitokeza kupiga kura ni ndogo sana hasa ikizingatiwa kuwa serikali ilitangaza siku ya mapumziko na hata kutoa usafiri bila malipo ili kuwawezesha watu wengi kupiga kura.

Mkuu wa zamani wa jeshi Abdel-Fattah el-Sisi anatarajiwa kushinda uchaguzi huo dhidi ya mpinzani wake mkuu Hamdeen Sabahi.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii