Mume amshtaki mkewe kwa kumnyima ngono

Image caption Majaji waliamua kuwa mkewe Mason hakufanya kosa lolote

Kuna kisa kimeibuka nchini Uingereza ambapo mwanamume mmoja kwa jina David Mason, mwenye umri wa miaka 30, alimshitaki mkewe Brenda kwa kumnyima haki yake ya kingono au kukataa kushiriki tendo la ndoa.

Mwanamke huyo alimfanyia mgao wa wiki moja kila mwezi wa kitendo cha ndoa mumewe kwa hofu ya kushika mimba kwa mara ya tatu.

Kwa mujibu wa jarida la mtandao la Mirror, la Uingereza, Bwana Mason, ambaye kazi yake ni fundi mitambo alishinda kesi hiyo mwaka 1980.

Lakini mkewe alikataa rufaa ambapo Mason alipoteza kesi hiyo baada ya majaji kusema kuwa mahakama isingeweza kuamua kuwa mkewe Mason alimkosea.

Nini maoni yako kuhusu tukio hili?